Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri
mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi
alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii,
Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa
mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa
mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti
Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi
Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja
la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja
ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa
kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo
daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la
ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la
iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha
mkuu iii na Afisa vipimo.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa
ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga
na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.
Nafasi
nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji
Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe
na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.
Nafasi
hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri
ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi
Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Ushetu.
Waajiri
wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi,
Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi
Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale,
Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.
Nafasi
hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro,
Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Ruangwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hai.
Katika
nafasi hizo waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa na
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bahi,
Waajiri
wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi
Halmashauri Manispaa ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani,
Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa
Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza,
Katibu Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa
Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa,
Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa
Njombe, Katibu Tawala Mkoa Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.
Daudi
amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 10 Desemba,
2013. Aidha amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba
Kila mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali
eneo au mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi
ya waombaji katika eneo husika.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Novemba, 2013.