Higuain ameizamisha Arsenal na chini Arteta akionyeshwa kadi nyekundu. Angalia na msimamo chini.
ARSENAL
ilipata pigo dakika ya 76, nahodha wake, Mikel Arteta alipotolewa nje
kwa kadi nyekundu na mwisho wa mchezo ikafungwa 2-0 na Napoli ugenini
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa imefanikiwa kufuzu hatua ya 16
Bora.
Mabao ya Napoli yamefungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 73 Callejon dakika ya 90.
Mabao ya Napoli yamefungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 73 Callejon dakika ya 90.
Neymar amepiga hat trick yake ya kwanza Ulaya
Katika
mchezo mwingine, Barcelona licha ya kuwakosa Andres Iniesta aliyebaki
benchi, Leo Messi ambaye bado majeruhi na Cesc Fabregas anayetumikia
adhabu, imeichapa mabao 6-1 Celtic.
Neymar aliyeongoza safu ya
ushambuliaji hakufanya makosa baada ya kufunga hat trick yake ya kwanza
katika Ligi ya Mabingwa dakika za 45, 48 na 58, wakati mabao mengine
yalifungwa na Pique dakika ya saba, Pedro dakika ya 39, na Tello dakika
ya 72.
Bao pekee la Demba Ba dakika ya 11, limempa faraja kocha Jose Mourinho wa Chelsea kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Steaua Bucharest.
Mapema mchana wa jana katika mchezo wa kiporo, bao pekee la Wesley Sneijder liliipa ushindi wa 1-0 nyumbani Galatasaray dhidi ya Juventus na kufuzu 16 Bora, huku Kibibi Kizee cha Turin kikifungishwa virago.(P.T)

Drogba akishangilia na Sneijder baada ya kuivusha 16 Bora Galatsaray
Katika
mechi nyingine za usiku huu, Marseille imefungwa 2-1 nyumbani na
Borussia Dortmund, Atletico de Madrid imeidunga 2 - 0 FC Porto, FC
Schalke 04 imeifunga 2 - 0 Basel, FK Austria Wien imeifunga 4-1 Zenit St
Petersburg, AC Milan imetoka sare ya 0-0 na Ajax.