MSANII
filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu
kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki
nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali
ni mfanyabiashara.
Madaha
amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kamwe huwezi kumlinganisha na
msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana
na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii wa
ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
Baby
madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema
kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio
huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina
makubwa hususani wasanii.
Akizungumza na kandili yetu
katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, "Binafsi
niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii
Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo.
kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo
lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake
liendelee kuwika".
"Siku
wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa
penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa
sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza
kuporomoka"alifafanua Baby Madaha