Yanga wamelipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 kama ada ya uhamisho na kumsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili.
Okwi anatarajia kuwasili nchini hivi karibu akitokea Uganda, ameiomba Yanga abaki nchini Uganda kumalizia kufanya tangazo la kampuni moja ya simu nchini humo.
Hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC ) imepatikana leo saa tisa mchana.