Hayati Arafat huenda hakuuawa kwa sumu

 3 Disemba, 2013 - Saa 16:30 GMT


Wapalestina wamekua wakisisitiza kuwa Aarafat aliuawa na Waisraeli
Kikundi cha madaktari wanaochunguza kifo cha hayati Yasser Arafat kilichotokea mnamo mwaka 2004, wanasema kuwa huenda Arafat hakufariki kutokana na sumu.
Kulingana na taarifa zilizofichuliwa nchini Ufaransa, wataalamu hao wameelezea kuwa Arafat alifariki kutokana na ugonjwa wa kawaida.
Ripoti hii inakinzana na taarifa ya awali ya watalaamu kutoka nchini Uswizi, waliofanyia utafiti mabaki ya Arafat, na kuelezea kuwa ulikuwa na kiwango kikubwa cha sumu kali aina ya Polonium.
Taarifa hiyo bila shaka ilithibitisha madai kuwa Arafat aliyekuwa rais wa wapalestina kwa mda mrefu, aliuawa kwa sumu.
Stakabadhi rasmi kuhusu afya ya Arafat, zilionyesha kua alifariki mwaka 2004 kutokana na kiharusi kilichosababishwa na maradhi ya damu.
Madaktari nchini Ufaransa, hata hivyo walikuwa wameshindwa kubaini kilichosababisha maradhi ya damu.
Mwili wake ulifukuliwa na kufanyiwa uchunguzi mwaka jana huku madai yakikithiiri kuwa hayati Arafat aliuawa kwa sumu.
Wapalestina wengi wameituhumu serikali ya Israel kwa kusababisha kifo cha Arafat madai ambayo Israel imekuwa ikikanusha.
Mwaka 2012,mnamo mwezi Julai, shirika la habari la al-Jazeera liliripoti katika mojawapo ya vipindi vyake kuhusu kifo cha Arafat na kusema kua wataalamu wa Uswizi, walipata kiwango kikubwa cha sumu aina ya Polonium katika mavazi ya Arafat aliyokabidhiwa mjane wake baada ya kifo chake.
Mjane wa Arafat aliiomba mamlaka ya Palestina kumruhusu kufukua mwili wa mumewe ili ukweli uweze kubainika na utawala huo ukaitikia wito wake.
Aidha maafisa wa Palestina wanasema kua hivi karibuni wataalamu wake wataweza kuwataja watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Arafat .
 source: BBC swahili

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger