Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo
Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea
wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo
kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu kutokana na
kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.
Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo
zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na
kwamba mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri
hiyo kwani madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM
kwa tuhuma za kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo
Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa
karibnu na kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za
Mitaa mwakani.
CREDIT : Mwananchi
CREDIT : Mwananchi