Kuhusu
hili tukio, Kamanda wa Polisi Kinondoni anasema ‘December 11 2013 saa
nane mchana maeneo ya Maringo roundaboutJaphet Mriga ambae ni Mwanajeshi
wa JWTZ Lugalo akiwa na mwenzake ambae ni mfanyabiashara Abdul
Zacharia, walikua wanatoka bank ya NMB Mlimani City ambapo Mwanajeshi
huyu alichukua shilingi milioni tisa kwa dhumuni la kumpatia Zacharia
ili amnunulie gari Zanzibar’
‘Sasa walipofika maeneo ya Maringo walivamiwa na Majambazi watatu wakiwa na pikipiki na walifanikiwa kumpora Mriga fedha na katika purukushani walimjeruhi Mwanajeshi huyu kwa risasi kwenye paja na kiganjani, wakati yote hayo yakiendelea Majambazi hawa walipigana risasi wao kwa wao ambapo jambazi mmoja alipigwa risasi kwenye mbavu upande wa kulia na kufariki papohapo na kupatikana akiwa na bastola moja yenye risasi 6′ – Kamanda
Kwa kumalizia, Kamanda amethibitisha kukamatwa kwa pikipiki moja iliyokua ikitumiwa na Majambazi ambapo msako mkali unaendelea kuwatafuta wale Majambazi wengine waliotoroka wakiwa na silaha nyingine ambayo ndio imemuua Jambazi mwenzao na kumjeruhi Mwanajeshi Mriga ambae alipata matibabu hospitali ya Lugalo na sasa anaendelea vizuri.
Mwili wa Jambazi alieuwawa akiwa na kofia ya kuendeshea pikipiki.
Pikipiki iliyokua ikitumiwa na Majambazi.
Mwanajeshi aliejeruhiwa.
Wananchi wakishangaa kwenye eneo la tukio.
Gari ya Polisi ikichukua mwili wa Jambazi pamoja na kumbeba Mwanajeshi aliejeruhiwa.