Gari maalum lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Nelson Mandela likitokea Hospitalini na msafara kuelekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya watu maarufu kutoa heshima za mwisho.
Raia wa Afrika Kusini wakiwa wamejipanga kando kando ya barabara kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Nelson Mandela.
Mwili wa Mzee Nelson Mandela ukiwasili kwenye jengo lililopo mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria, ambapo utalala kwa siku tatu kuruhusu Raia wote wa Afrika Kusini na Dunia kwa ujumla kutoa heshima zao za mwisho.
Mke wa kwanza wa Mzee Nelson Mandela akionekana na majonzi mazito akielekea kutoa heshima za mwisho kwa mumewe wa zamani.
Mwanamindo wa Kimataifa Naomi Campbell alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuona jeneza la Mzee Nelson Mandela likiwasili kwenye viwanja hivyo tayari kwa kutoa heshima za mwisho.
Rais Jacob Zuma na mkewe wakitoa heshima za mwisho.(HD)