Kenya imeanza sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa hilo
huku wananchi wake wakitaabika na adha ya kupata matibabu kutokana na
mgomo wa madaktari ambao leo hii unaingia siku yake ya pili.
Madaktari wanaishinikiza serikali wapate maslahi bora kwa mujibu wa
katiba mpya ya taifa hilo. Kutoka mjini Nairobi Sudi Mnette amezungumza
na mchambuzi wa siasa za Kenya, Barack Muluka na kwanza alitaka kujua
nini hasa kiini cha mgomo huu wa sasa. Kusikiliza mazungumzo hayo
bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini