Estelina Sanga ‘Linah’. |
Akizungumza na mwandishi wetu Desemba 9, mwaka huu jijini Dar, Linah alisema tangu alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria kushika ujauzito kwa kuwa alikuwa bado hajajiandaa kufanya hivyo.
Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama katika penzi zito la staa mwenzake, Amin Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni tofauti na anataka kuzaa iwapo atashika ujauzito.
“Nilipokuwa katika uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu aliponiambia tuzae nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike mimba na ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba,” alisema Linah.
Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi uhusiano wake wa sasa na hakutaka kumwongelea Amin.