Katika kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 1,475.
Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Emmanuel Nchimbi imesema wafungwa watakaonufaika na msamaha huo wa rais ni wale wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wako kwenye hali mbaya. Wengine ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 walioingia kifungoni na mimba na wale wenye watoto wachanga na wale wenye ulemavu wa mwili na akili.
Aidha msamaha huo wa raia hautawahusu waliohukumiwa kunyongwa au wanaotumikia kifungo cha maisha, wanaotumikia kifungo kutoka na makaosa ya biashara ra ya dawa za kulevya , rushwa, wizi na unyang’anyi wa kutumia silaha , waliobaka, kunajisi au kulawiti, wezi wa magari na wale waliowapa mimba wanafunzi.
Wengine ni wale waliofungwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na wale waliowahi kutoroka wakati wa kifungo.