"Siwezi kushindana na DIAMOND kwasababu mimi sio Mwimbaji"...WEMA
Je wewe ni kati ya wanaoamini kuwa wapenzi ‘wa zamani’ Wema Sepetu na Diamond Platnumz wanashindana kwa namna yoyote? Star wa kipindi cha ‘In My Shoes’ Wema Sepetu ameshare ujumbe kwa wote wanaofikiria hivyo.
Kupitia Instagram ameandika kuwa kitu pekee kinachosababisha watu wahisi hivyo ni kutokana na wote wawili kuwa na mafanikio katika fani zao (muziki na movie), na kuongeza kuwa hawezi kushindana na Diamond sababu yeye sio muimbaji.
Source: Bongo 5