Asikwambie mtu, wanaume wengi wa Kiafrika wanapenda sana mwanamke kuwa na chachandu kwani wanakwambia zinawapa raha na utulivu wanapokuwa faragha.
Chachandu zinapaswa kuvaliwa wapi?
Leo
ni wengi wanataka kujua zinavaliwa wakati gani, shosti si kila sehemu
unavaa chachandu angalia na sehemu ya kuzivaa kwa sababu ukizivaa eneo
la kazi utatafsiriwa vibaya, zile zinafaa kuvaliwa chumbani ukiwa na
mpenzi wako tu.
Unajua
zile zinatungwa na uzi huenda ukazivaa na ikatokea zikakatika hivi
utajisikiaje ukiwa sokoni halafu zikakatika lazima utaona aibu na
wengine hudiriki kuziacha hapohapo. Cha kufanya shosti yangu vaa kwa
raha zako wakati unahisi mumeo anataka kurudi nyumbani, ukishaoga na
umeshajiandaa kwa kumpokea mume unaweza kuvaa chachandu kwani
zitachangia kumuweka tayari mumeo.
Rangi za chachandu na maana zake
Ukiachia
mbali kunakshi kiuno chako pia zinamaana kwa rangi mojamoja ingawa siku
hizi wanawake wamekuwa wakichanganya rangi kwa ajili ya mapambo tu na
kumvutia mume lakini kuna rangi ambazo ni viashirio vya lugha ya
kuwasiliana na mwenzako pale utakapotaka abaini jambo fulani na maana
hizi ndiyo nakuletea shoga yangu.
Rangi
kama pinki, bluu, dhahabu hizi rangi hazina maana kwenye sita kwa sita
ni urembo tu kupendezesha kiuno, hukatazwi kuzivaa shosti sasa
ninazokufundisha ni hizi.
Nyekundu
Ukimkuta
mwanamke amevaa chachandu ya rangi hii unatakiwa kuelewa kwamba
mwanamke huyu yupo kwenye hedhi, kwahiyo wewe fanya mengine lakini siyo
safari ya kupeana maraha kwani kwa kufanya hivyo kiafya si vizuri
unatakiwa kuwa mpole tu.
Nyeupe
Ukimkuta
mwanamke amevaa chachandu nyeupe hii humaanisha hana tatizo lolote
litakalomfanya asikupe raha ya sita kwa sita, kwa hiyo ukitaka tu muda
wowote unapata kwani anakuwa amejipanga kwa lolote.
Nyeusi
Ukimkuta
mwanamke amevaa rangi hiyo, humaanisha ya kwamba yupo tayari kukupa
raha za sita kwa sita lakini uwanja wake haujakatwa majani, kwa hiyo
chaguo ni lako kama unataka kutumia siku nzima kutafuta goli haya, ama
kama utamsaidia kumkatia majani uwanjani vizuri zaidi ama kama huwezi
yote basi mpe muda akate mwenyewe.
Hitimisho
Wanawake
wa zamani walikuwa hawavai chachandu, wanatandika sita kwa sita vizuri
kisha wanatupia rangi wanayoona inamfaa kwa siku hiyo, baba akitoka
safari anakuta chachandu ya rangi nyekundu iko kitandani anajua mkewe
alikuwa anatumikia siku zake siku zinaenda.
Mashosti kuna wengine hawapendi kuvaa kabisa unaweza kutumia kwa kuitupia ile unayoona inakufaa kumfikishia ujumbe mume wako kwa siku hiyo, lakini kumbuka kwa kuivaa inaleta hamasa fulani na kukusaidia kumuweka karibu mumeo