KUNA
mambo ambayo yanaweza kuonekana ya kawaida tu au si ya lazima sana
lakini kumbe yana uzito na thamani kubwa sana kwenye uhusiano. Wengi
wakitaka kufanya jambo la kumfurahisha mpenzi wake, huwaza katika
ukubwa.Wapo
wanaofikiri labda kwa kutoka na mwezi wake kwenda naye kwenye hoteli
kubwa ya kifahari ya nyota tano na kulala kwa usiku mmoja lina thamani
kubwa. Pengine wapo wanaofikiri kuwa, kuwanunulia wenzi wao vitu vya
thamani kubwa kama cheni ya dhahabu, gari n.k ndivyo vyenye thamani
pekee!
Si kweli. Ni ukweli usio na shaka kwamba, mwanamke anapenda kufanyiwa
vitu vyenye thamani na mwanaume wake. Ukweli unabaki kuwa, wakati
mwingine unaweza kuwa unatamani kumfanya mwenzi wako awe na furaha muda
wote lakini mfuko wako ukawa hauruhusu!
Hulka ya wanawake wengi ni kutamani kuona mwenzi wake anamuona ni mtu
muhimu na anakuwa naye karibu muda wote. Wanawake hawajali sana vitu
vya thamani kama wanaume wanavyofikiri.
Kumkumbatia mwanamke na
kumbusu katikati ya midomo yake, ukisindikiza na maneno matamu ni zaidi
ya gari utakalomnunulia – kikubwa hapa, mwanamke huyo awe kweli ana
upendo nawe na si kuwa yupo kibiashara!
Katika mada hii, nimekuandalia vitu vichache ambavyo kwa hakika, kwa
mujibu wa utafiti nilioufanya, ni ‘sumu’ kwa wanawake. Ukifanya vyote au
sehemu yake, unamfanya mwanamke wako ajihisi yupo katika mikono salama.
Bado
thamani ya mali na vitu vingine vitabaki katika uhalisia wake, lakini
kwa hakika mambo yafuatayo hapa chini, huwachanganya sana wanawake.
KADI
Ni utaratibu uliozoeleka sana kipindi cha
nyuma kidogo. Sasa hivi teknolojia imeongezeka, kadi inaweza kupatikana
hata kwenye mitandao mbalimbali ya internet. Hata hivyo, bado inaonekana
kuwa mwanamke anapenda na anatamani kuona mwanaume wake anamkumbuka kwa
kumtumia kadi.
Wanaume wengi ni wavivu, lakini kwa sababu ya ustawi wa penzi lako,
jaribu hili. Nunua kadi yako yenye ujumbe mzuri, andika maneno mengine
kwa mkono wako mwenyewe, pulizia manukato unayotumia, kisha mtumie/
mpelekee mpenzi wako. Utakuwa umemroga!
NYIMBO, MASHAIRI
Wanawake wanapenda sana kufahamu
kuwa kweli alipo anapendwa. Nyimbo nzuri za mapenzi ambazo zitaeleza
uzuri wake na namna unavyompenda na kumthamini, vinazidi kukuweka katika
kilele cha umiliki uliotukuka.
Mchagulie mpenzi wako wimbo redioni,
taja jina lake, lako na ujumbe wako. Utamfanya ajisikie fahari sana.
Mashairi katika magazeti mbalimbali na majarida pia huongeza ladha ya
mapenzi.
Anachojali mwanamke ni ile hali ya kuona kuwa, unampenda na unaweza
kuthibitisha hilo hata mbele ya watu wengine. Kusikia akitajwa redioni
au ameandikwa gazetini ukionyesha hisia zako za kumpenda, kutamchanganya
na kumfunga kabisa hisia za kufikiri kukusaliti.
Tatizo wanaume wengi hawatilii maanani haya mambo lakini kama unataka kuwa dume la mbegu kwa mwanamke wako, jaribu uchawi huu....itaendelea.