Wazanzibari waling’olewa jana Alhamisi baada ya Rwanda kuifunga Eritrea bao 1-0 mjini Machakos.
Zanzibar ambayo ilimaliza mechi zake Jumanne ikiwa
na pointi tatu ilikuwa ikisubiria mechi ya jana ili kujua kama
watapenya kwa tiketi ya upendeleo ya Cecafa ambayo ilikuwa ikiwaniwa na
Burundi, Rwanda na Zanzibar.
Kocha wa Zanzibar, Salum Bausi amelalamikia
kitendo cha mechi za mwisho kuchezeshwa kwa siku tofauti badala ya
kuchezeshwa siku moja.
Kwa upande wa Stars ambayo ilifuzu juzi Jumatano
baada ya kuichapa Burundi bao 1-0, itacheza na Uganda ambayo imeongoza
kundi C baada ya kuifunga Sudan bao 1-0 jana kwenye Uwanja wa Nyayo.
Bao la Uganda lilifungwa katika dakika ya 57 na Khalid Aucho, huku la Rwanda likifungwa na Ndaihuka Michel katika dakika ya 70.