TAZAMA JINSI KASEJA ALIVYOKUSANYA KIJIJI MAZOEZINI YANGA


Na Waandishi Wetu
NGUVU ya nyota ya kipa Juma Kaseja imeendelea kung’ara katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi yaliyofanyika juzi na jana, rundo la mashabiki ‘kijiji’, liliacha kuangalia mazoezi ya wachezaji wa ndani na kuhamia alipokuwa Kaseja.
Mashabiki hao walionyesha wamepania kumuona kwa karibu, hivyo idadi kubwa walihamia upande aliokuwa akijifua pamoja na kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, wote wakiwa chini ya kocha wao, Razak Siwa, raia wa Kenya.
Awali, mashabiki hao walikuwa upande mmoja wakishuhudia mazoezi ya Yanga kwa ujumla, lakini walipoona mazoezi ya makipa yameanza, wote walihamia huko huku kila mmoja akisisitiza alitaka kumuona Kaseja akijifua.
Pamoja na nyota yake kung’ara zaidi, Kaseja alionekana kuchoka sana na baadaye Siwa alisema ilitokana na kutofanya mazoezi kwa kipindi kirefu.
“Amejitahidi sana, wengine huishia katikati,” alisema Siwa.
Baada ya hapo, timu zilipangwa na Kaseja na Barthez, kila mtu akachukua milingoti miwili.
Hadi mwisho wa mazoezi, Kaseja alifungwa bao moja huku Barthez akifungwa mawili na timu yake kulala kwa 2-1.
Didier Kavumbagu na Simon Msuva ndiyo walimtungua Barthez na mkongwe Nizar Khalfan akamtungua Kaseja.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger