WABUNGE 375 WANUNULIWA IPAD KWA FEDHA ZA UMMA,ZAIDI YA MILIONI 590 ZA KITANZANIA ZATUMIKA.....


Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa za Umma. Afisa mkuu wa Bunge amesema kuwa tabiti hizo zitawafanya wabunge kuwa makini wakati wa vikao vya bunge. Kamishna wa bunge Emmanuel Dombo amesema kuwa wabunge sasa wanaweza kupata stakabadhi zao rasmi wakati hata wakiwa nje ya ofisi zao au wakiwa safarini.

Pia alisema kuwa pesa walizonunulia iPad hizo zitasaidia kuepuka kutumia kiwango kikubwa cha karatasi na kupunguza gharama ya matumizi.
Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha dola laki tatu na sabini.
Wakosoaji wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua hata kuzitumia tabiti hizo na kusema kuwa tayari wananchi wanalipa pesa nyingi sana kwa mishahara ya wabunge
Mwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa kwa asilimia arobaini.
Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola 40,000 ili kujinunulia gari jipya.
Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.
Wananchi wanasema kua hatua hii ya serikali ni kuharibu pesa za mlipa kodi, ikizingatiwa kuwa wabunge hao wanalipwa mishahara ya juu ambayo inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo wao wenyewe.

BBC SWAHILI

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger