Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha dola laki tatu na sabini.
Wakosoaji wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua hata kuzitumia tabiti hizo na kusema kuwa tayari wananchi wanalipa pesa nyingi sana kwa mishahara ya wabunge
Mwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa kwa asilimia arobaini.
Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola 40,000 ili kujinunulia gari jipya.
Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.
Wananchi wanasema kua hatua hii ya serikali ni kuharibu pesa za mlipa kodi, ikizingatiwa kuwa wabunge hao wanalipwa mishahara ya juu ambayo inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo wao wenyewe.
BBC SWAHILI