HII NDIO TAARIFA KAMILI KUHUSU MTANGAZAJI WA TBC FM ALIYEKOSWAKOWA KUWAWA NA SIME...!




AMA kweli nimeamini Maisha ni Watu na siku zote Tenda Wema Nenda zako.

Huyo jamaa aitwae Bondia Mada Maugo maskani yake Gongo la Mboto.Jana alikuwa na Uzinduzi wa Wimbo wake aloimbiwa na Bendi ya Kijaluo.

Nilienda hapo kumsapoti mpaka nikanunua CD 1 kwa SH 50000.Yote hayo ni kwa ajili ya kumpa yeye Sapoti na hata hivyo mimi huwa nampa sana sapoti anapokuwa na mechi zake pamoja na kuwa anaishia kutwangwa,ila kumbe fadhila za Punda ni Mateke.

STory iko hivi,jana baada ya Uzinduzi wa hiyo CD wakati wa kuondoka Dem wake tena akiwa na Yeye Maugo akaja kuongea na mimi akidai anasoma Chuo Cha Utangazaji hivyo angefurai kama ningempa sapoti ya kufanya fild TBC fm na akadai anapenda Sana Vipindi vyangu hivyo lets be intouch.

Akiwa anazungumza na mimi alikuwa akiongea kiingereza,sasa sikujua labda Mada alijua Dem wake ananitaka au la.Si unajua tena Mwenzangu na mimi hajui hata ya kuombea maji,hiyo lugha imempita kushoto.

Jamaa akaanza kufoka na kuanza kumpiga Dem wake,Akaona haitoshi Kachukua sime kwa gari eti anakuja kunichoma nayo.

Bahati nzuri kulikuwa na Watu pale Wakamshika.Ila Poa Pamoja na yote mimi kwa Roho Safi nimemsamehe coz yule mtu na Chizi hakuna utofauti.Ngumi anazopigwa zimemfanya awe Chizi.Kwa Wanaomjua Vizuri watakubaliana na mimi

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger