Baby Madaha msanii wa Filamu na muziki akiwa na rafiki yake.
MWIGIZAJI na msanii wa filamu Swahiliwood Baby Madaha amekubwa na kashifa kama si kituko kilichotokea hivi karibuni kati ya moja ya sehemu za starehe baada ya kufumwa na mapararazi akiwa kapagawa kwa kumlazimisha mwanamke mmoja kumpiga denda hadharani watu wakishangaa
Baby Madaha akiwa na mtu anayesadikiwa alikuwa akimla denda Bar.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kwenye na Bar ya Uhuru Peack
iliyopo maeneo ya Vijana sehemu ambayo akipata moja baridi moja moto
Baby Madaha ambaye alikuwa tungi kupita kiasi alianza kumlazimisha dada
huyo kumla mate baada ya kumsifia kwa kazi nzuri anazozifanya msanii
huyo.Baby Madaha alipotafutwa na kuulizwa kuhusu tukio alisema hajui na wala hana kumbukumbu kama aliwahi kufanya tukio kama hilo kwa sababu yeye ni mtu anayejiheshimu na hawezi kufanya ujinga huo mbele ya kadamnasi wakati yeye anajua kuwa ni mtu maarufu.
“Sijui nani analeta habari hizo katika vyombo vya habari lakini lazima wafahamu kuwa mimi ni mtu makini ninajiheshimu pia ni kio cha jamii so siwezi kufanya vitu kama hivyo tena Public no siwezi najielewa,”anasema Baby Madaha.
Msanii huyo wa filamu na muziki amekuwa akifanya vizuri katika sehemu zote mbili yaani filamu na muziki ambapo hivi karibuni ameingia mkataba na kampuni ya muziki yenye makazi yake nchini Kenya.