Katika
hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni
jijini Dar, (28) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya
kuchomwa sindano inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia kujihusisha kimapenzi
na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wa askari Polisi.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Elias alidai
alikumbwa na mkasa huo mwaka 2011 wakati akiwa na uhusiano wa kimapenzi
na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Amina, ambaye pia alijihusisha
na polisi aliyemtaja kwa jina moja la James, aliyekuwa akifanya kazi
katika kituo cha Polisi cha Kilwa Road, jijini Dar es Salaam.
“Polisi huyo alikuwa akinifuata mara kwa mara na kuniambia kuwa
niachane na mwanamke huyo, lakini kwangu ilikuwa ngumu kwa sababu
tulipendana sana,” alisema kijana huyo.
Alisema siku ya tukio, akiwa kijiweni, polisi huyo akiambatana na wenzake, walifika na kumkamata bila kosa lolote na kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi Mianzini, Temeke.
Akiwa hajui hatima yake, Elias alisema mara tu baada ya kuchomwa sindano hiyo, alisikia maumivu makali yaliyopanda hadi kichwani na ghafla akapoteza uwezo wake wa kuona. “Siwezi kuelezea zaidi maumivu niliyoyapata baada ya kuchomwa sindano ile na hapo hapo macho yangu hayakuweza kuona tena licha ya kujitahidi sana,” alisema.
Alisema siku ya tukio, akiwa kijiweni, polisi huyo akiambatana na wenzake, walifika na kumkamata bila kosa lolote na kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi Mianzini, Temeke.
Elias John katika pozi akiwa na fimbo yake ya watu wasioona.
Wakiwa kituoni hapo, kijana huyo alisema kwa pamoja Polisi hao
walimshika mikono na miguu wakati James alichukua sindano na kumchoma.Akiwa hajui hatima yake, Elias alisema mara tu baada ya kuchomwa sindano hiyo, alisikia maumivu makali yaliyopanda hadi kichwani na ghafla akapoteza uwezo wake wa kuona. “Siwezi kuelezea zaidi maumivu niliyoyapata baada ya kuchomwa sindano ile na hapo hapo macho yangu hayakuweza kuona tena licha ya kujitahidi sana,” alisema.
Macho ya Elias yalivyoharibiwa na sindano inayodawa kuwa ya sumu.
Alisema baada ya kuchomwa sindano hiyo, askari hao walimtaka aondoke
na akajitahidi kuwapa taarifa ndugu zake, ambao walimchukua na kumpeleka
Muhimbili ambako hata hivyo walishindwa kumsaidia na hata alipopelekwa
CCBRT, pia ilishindikana.
Katika hali ya kusikitisha zaidi, ndugu zake walijaribu kufuatilia
suala hilo polisi, lakini walipofika waliambiwa kirahisi kwamba askari
hao wote walishafukuzwa kazi.
Alisema juhudi za ndugu zake kuhakikisha haki inatendeka zimegonga
mwamba licha ya suala lake kufikishwa kwa taasisi za haki za binadamu
ambako bado linashughulikiwa, ingawa hakuna matumaini ya kupatikana kwa
ufumbuzi.
“Maisha yangu yamekuwa magumu sana na sijui hatma ya kesi yangu,
nitaendelea kuishi hivi mpaka lini? Kwa vile kwa sasa naombaomba tu,”
alisema.
Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuliangalia suala lake kwa undani ili lipatiwe ufumbuzi.