"Zitto Anipe majina ya Vigogo walioficha Mabilioni Uswiss ili nimsaidie kuwataja...Sihitaji Kinga yeyote ile".....LEMA

Dodoma, Tanzania. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati akichangia  taarifa ya Kamati ya Sheria na Katiba muda mfupi uliopita  amemtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazni Zitto Kabwe kumkabidhi AG majina ya watu wote walioficha fedha Uswis ambayo alisema anayo.

 
Lema ameliambia Bunge kama Zitto na serikali wameshindwa kuwataja watu hao, wampe Lema majina hayo ili awataje.

Amefafanua kwamba hatahitaji kinga yeyote kuwataja wezi hao walioficha fedha Uswis ndani ya Bunge au nje ya Bunge.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger