>>RASMI ZAPANGWA KWENYE VYUNGU VYA DROO!
FIFA
leo imetangaza mwongozo wa jinsi Droo ya kupanga Makundi ya Fainali za
Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 Mwakani
zitakavyofanyika.
Fainali hizo zenye Nchi 32 zitapangwa katika Makundi 8 ya Timu 4 kila moja.
Katika mwongozo huo, FIFA imesema Timu 8
za juu kwa Ubora Duniani [Kwa mujibu wa Listi iliyotoka Oktoba], pamoja
na Wenyeji Brazil, zipo Chungu Namba 1 na zitapangwa kuanzia Kundi A
hadi H ili kuzitenganisha.
Brazil, kama Wenyeji, tayari wamewekwa
Kundi A na watacheza Mechi ya Ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia hapo
Juni 12 huko Sao Paulo.
-CHUNGU NAMBA 1: Brazil, Spain, Argentina, Belgium, Colombia, Germany, Switzerland, Uruguay
-CHUNGU NAMBA 2: Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria, Cameroon, Chile, Ecuador
-CHUNGU NAMBA 3: Japan, Iran, South Korea, Australia, United States, Mexico, Costa Rica, Honduras
-CHUNGU NAMBA 4: Bosnia, Croatia, England, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, France
FAHAMU: Kabla Droo
kufanyika itafanyika Droo maalum kuihamisha moja ya Timu za Ulaya toka
Chungu Namba 4 na kuiweka Namba 2 ili kuleta uwiano wa Nchi toka Mabara
tofauti.
Pia, Timu 4 za kutoka Marekani ya
Kusini, Brazil, Uruguay, Colombia na Argentina zitawekwa kwa muda Chungu
Namba X. Timu 3 ambazo hazitapangiwa ile Timu ya Ulaya ambayo
ilipelekwa Chungu Namba 2 zitarudishwa kwenye Droo kubwa kama
walivyopangiwa awali.